how to sell online

KADILO ONLINE
Umaskini ni chanzo kikubwa cha ukosefu wa afya bora katika jamii

UMUHIMU KUZINGATIA MLO KAMILI NA KUFANYA MAZOEZI UNAKUSAIDIA KUONDOA MSONGO WA MAWAZO, KUPUNGUZA UZITO, KUJENGA MISULI NA KUKUFANYA UJISIKIE VIZURI KATIKA SHUGHULI ZA KILA SIKU
Jinsi ya kuuza bidhaa au huduma mtandaoni!
Idadi kubwa ya watu hivi sasa wanapatikana kwenye mtandao, kwa wafanyabiashara ni fursa kubwa kuuza bidhaa au huduma mtandaoni.
Licha ya kuwa kuuza bidhaa au huduma mtandaoni kunahitaji ujuzi, lakini kanuni za kufanya biashara zinabaki pale pale.
Mfanyabiashara anayetaka kuuza bidhaa au huduma mtandaoni anahitaji kujifunza maarifa kidogo ya jinsi ya kuweza kufanyabiasra mtandaoni.
Kabla ya kueleza jinsi ya kuuza bidha au huduma mtandaoni ntakuleza kwanza jambo moja la msingi la kuzingatia kabla ya kufikiria kuanza kuuza bidhaa zako mtandaoni
Wazo la biashara
Kwa kifupi wazo la biashara ni wazo la kipekee linalohusisha mchakato wa kubuni bidhaa au huduma itakayolenga kutolewa kwa kundi fulani la watu kwa lengo la kutengeneza pesa.
Bidhaa au huduma mpya, wazo lolote la biashara jipya linalokuja na utatuzi wa matatizo ya kundi fulani la watu wenye matatizo yanayofanana ni wazo litakalokuwa na mafanikio kwenye bishara.
Wazo la bidhaa au huduma mpya linakuwa halina mshindani kwenye soko , haliwezi kupatikana kila mahali, _obvious_ litakuwa na thamani kubwa na kuweza kufanya vizuri kwenye biashara.
Kulenga ki-sehemu kidogo cha soko fulani, wazo linalolenga kundi fulani la watu wenye changamoto zinazofanana lina nafasi ya kufanya vizuri kuliko wazo linalolenga watu wote.
Mfano wazo la kuuza viatu, soko la viatu ni pana wazo la kuwauzia viatu watu wote haliwezi kufanya vizuri ushindani ni mkubwa vinapatikana kila mahali na thamani yake inashuka.
Lakini wazo la kuuza viatu kwenye soko fulani dogo la watu wenye changamoto zinazofana mfano kundi la kina wanawake wanaofanya kazi ofisi wanaotaka viatu _simple_ kwa ajili ya kupendeza ofisi.
Hilo ni soko maalum halina ushindani mkubwa.
Uvumbuzi wazo la biashara linalokuwa na ugunduzi wa kitu kipya au teknolojia mpya linakuwa na thamani kubwa kwa watu halipatikani kila mahali kwa kuwa ni kitu kipya.
*Upungufu katika soko*, wazo la biashara lililojikita kuangalia mapungufu katika soko fulani la watu kwa kuangalia hali ya kutokuwepo bidhaa au huduma na kutafuta suluhisho la hali hiyo ni biashara yenye mafanikio.
Katika somo lijalo tutaangalia jinsi ya kutathimini wazo la biashara ili kujenga biashara yenye mafanikio,ebu tuangali baada yakuwa na wazo zuri la biashara tunatakiwa kufanya nini kuanza kuuza bidhaa mtandaoni.
Kufanya biashara au kuuza bidhaa au huduma mtandaoni hauhitaji gharama kubwa, kunahitaji maarifa ya kujua namna ya kufanya kuweza kuteka soko lako kwenye mtandao.
Ukiweza kuuza bidhaa au huduma yako mtandaoni unakuwa umepanua wigo mkubwa wa biashara. Mabilioni ya watu siku hizi wako mtandaoni bidhaa na huduma nyingi zinafanyika mtandaoni.
Hapa ntazunguzia kupengele cha jinsi ya kutengeneza jukwaa mtandaoni kurahisisha mauzo mtandaoni.
Kwanza unatakiwa kutengeneza akaunti ya biashara kwenye mitandao ya kijamii au platform za kuuza bidhaa mtandaoni.
Baada ya kuwa na akaunti lipia tangazo ili upate watu wengi watakaona tangazo lako.Tangazo utakalo boost hakikisha halitangazi bidhaa au huduma liwe linatangaza jinsi ya kutatua changamoto ya wateja.
Gharama ya matangazo unaweza kulipia dola kumi sawa na wastaniwa sh30,000 kwa wiki kwenye facebook Baada ya kutangaza wakaribishe walengwa wako kwenye jukwaa lako na kuanza kuwaelimisha wateja kuhusu changamotoa zao.
Kumbuka kuwa wateja hawanunui bidhaa kwa sababu wanataka kununua kwako, wateja wananunua bidhaa au huduma kutatua changamoto zao ukiweza kueleza changamoto zao utaaminika na kuweza kupata wateja kirahisi mtandaoni.
Aidha wauzaji aliofanikiwa kufanya mauzo kwa kiasi kikubwa mtandaoni wamekuwa wakitengeneza mahusiano mazuri na wateja wako, jenga mahusiano na wateja wako kwa kuwa na orodha ya wateja wako na kuwasiliana nao mara kwa mara.
Jenga uaminifu, hapa wateja hakujui wahawakupendi, hawakuwami wanawezaje kununua bidhaa au huduma yako mtandaoni, unatakiwa kuhakikisha unajenga uaminifu kwa wateja kwa kupatikana muda wote pale wanapohitaji msaada kutoka kwako.
Vile vile ili kufanikiw kuuza bidhaa au huduma mtandaoni utanakiwa kuwa mkweli kwa kile unachokiuza, na kutengeneza kuaminika (authority), vipi watu watakuamini kuwa unaweza kutatua changamoto zao, utakiwa kutoa taarifa zinazogusa matatizo yao.
Comments
Post a Comment